PETER MSECHU AWAPONDA WASANII WANAOISHI KWA KUTEGEMEA "KIKI"

MSANII wa Bongo Fleva, Peter Msechu amewaasa wasanii kuacha kutegemea "kiki" wakati wanapotaka kutoa nyimbo zao kwa lengo la kufanya vizuri.

Msechu alisema kuwa, siku za hivi karibuni wasanii wanapotaka kutoa nyimbo wanatafuta pa kutokea kwa kufanya kitu ambacho kitawafanya wazungumzwe ndipo wanaachia nyimbo zao.

“Sidhani kama ni sawa, kama nyimbo nzuri lazima itakubalika tu si lazima kutumia kiki flani ndio utoe nyimbo, mi nadhani wasanii tungebadilika na kuachana na dhana hizo ambazo kwangu naziona zimepitwa na wakati,” alisema Msechu.


Msechu amesema yeye kama msanii makini amekuwa akifanya nyimbo zake kwa umakini mkubwa, hategemei kutoa nyimbo kwa kutumia kiki kwa kuwa anatambua kipaji chake.

No comments