PICHA 14: JAHAZI ILIVYOWEKA HESHIMA TRAVERTINE JUMAPILI USIKU ...funga kazi ni Dar Live Jumamosi hii


Inawezekana kabisa kuwa hii inakuwa ni rekodi mpya ya mahudhurio yaliyonona kwa Jahazi Modern Taarab ndani ya ukumbi wao wa nyumbani – Trvertine Hotel – tangu bosi wao wa zamani Alhaj Mzee Yussuf atangaze kuachana na muziki.

Naam show ya Jahazi Jumapili usiku hapo Travertine Hotel, ilishuhudiwa na umati mkubwa wa watu, idadi ambayo haijawahi kuonekana hapo kwa takriban mwaka mzima.

Show hiyo iliyosindikizwa na vikorombwezo kadha wa kadha ikiwemo kibao kata kutoka kwa Kivurande Junior, ilitosha kudhihirisha kuwa Jahazi bado ina hazina kubwa ya mashabiki na kinachotakiwa ni ‘fitna’ tu za kuleta ‘amsha amsha’.

Baada ya onyesho la Jumapili usiku, sasa nguvu zote za Jahazi zimeelekezwa Dar Live, Mbagala katika onyesho lingine kubwa kabisa la taarab litakalofanyika Jumamosi hii Agusti 5.

Katika onyesho la Dar Live mbali na Jahazi, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Zanzibar Stars Modern Taarab, Khadija Kopa, Khadija Yussuf, Dulla Makabila, Kivurande Junior na Hanifa Maulid "Jike la Chui"

Pata baadhi ya picha za onyesho la Jumapili usiku, lililoitikisa Travertine Hotel.
 Ally Jay akipapasa kinanda kwa mbwembwe
 Dida kutoka Times FM mmoja wa waratibu wa onyesho la Jahazi Jumapili usiku
 Dida akiwa na mashabiki wake
 Dr Kumbuka kutoka Times FM ndiye aliyekuwa MC wa show ya Jahazi
 Mwasiti Kitoronto akiimba "Nataka Jibu"
 Kivurunda Jr akipagawisha na kibao kata
 Wataalam wa kibao kata chini ya Kivurande Jr
 Kivurande akiimba wimbo wake "Moyo kama Macho"
 Dida na Dr Kumbuka wakionyeshana ufundi wa maneno
 Mtu na mtuwe ...Prince Amigo akiimba huku akipata kampani kutoka kwa mkewe
 Hii ndiyo taswira ya Travertine Jumapili usiku
 Amigo na mkewe
 Amigo akiimba "Tiba ya Mapenzi"
Travertine ilifurika kama hivi

No comments