PICHA 15 ZA MAPACHA WATATU YA CHOKORAA NDANI YA GARDEN BREEZE JUMAPILI ILIYOPITA …anyofoa wasanii wa Twanga Pepeta


Bendi ‘mpya’ ya Mapacha Watatu chini ya Khalid Chokoraa, Jumapili iliyopita, iliwasha moto wa burudani ndani ya ukumbi wa Garden Breeze, Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam.

Mapacha Watatu iliyokuwa na sura za wasanii wa kukodiwa kama na Said Ndagendage mpiga Kinanda wa Zanzibar Stars Modern Taarab, mwimbaji/rapa Frank Kabatano na mpiga bass Evans Mwaigomole wote kutoka TOT, ikatesa kwa program ya nyimbo mchanganyiko - za ndani na nje ya nchi.

Chokoraa akitengeneza safu ya uimbaji sambamba na Catty Chuma na January Elevan ambao wote waliwahi kushiriki na Mapacha Watatu ile ya mwanzo, wakafanikiwa kupiga nyimbo zote kali za Mapacha wakifukia vizuri sauti za Jose Mara na Kalala Jr.

Mbali na nyimbo za dansi, Mapacha Watatu iligonga hadi nyimbo za taarab ambapo wimbo “Njiwa Peleka Salamu” wa JKT Taarab, ulitendewa haki na Catty Chuma.

Kwenye drum alikuwepo Martin Kibosho, solo likashikiliwa na Super Black, safu ya wanenguaji ikaundwa na Sabrina, Otilia na Master B.

Lakini kubwa zaidi ni kwamba Chokoraa ambaye aliahidi kutotumia wasanii wa Twanga Pepeta, mbali na kukiuka kali yake kwa kuwachukua Otilia na Master B, pia amemjumuisha Amani “Rasi”, kijana anayetoka ndani kabisa ya familia ya kina Asha Baraka.


Amani kwa miaka mingi alikuwa ndiyo mtu anayesimama getini kwenye show za Twanga Pepeta na kupokea tiketi, lakini Chokoraa alimjumuisha katika show yake ya Jumapili na kumtupa kwenye safu ya waimbaji wa Mapacha Watatu. Kipaji kipya kimevumbuliwa.
 Evans kwenye gitaa la bass
 Catty Chuma kwenye safu ya uimbaji
 Khalid Chokoraa boss wa Mapacha Watatu
 Catty Chuma "First Lady"
 Sabrina mmoja wa madansa wa Mapacha Watatu
 Amani "Rasi" akiunda safu ya waimbaji wa Mapacha Watatu
 January Eleven na Chokoraa
 Frank Kabatano
 Martin Kibosho kwenye drums
 Ndagendage kwenye kinanda
 Sabrina na Otilia
 Otilia, Sabrina, Master B kwenye safu ya unenguaji
 Super Black kwenye solo. Nyuma yake ni fundi mitambo Masoud ambaye pia hutumiwa na Twanga Pepeta
January Eleven akiimba kwa hisia kaliNo comments