Habari

PICHA 15 ZA SHOW BAB KUBWA YA FM ACADEMIA NA MASHAUZI CLASSIC NDANI YA NEFALAND HOTEL IJUMAA USIKU

on

Ijumaa usiku
ndani ya ukumbi wa Nefaland Hotel, Magomeni Kagera jijini Dar es Salaam,
ilipigwa show ya kutakata kutoka kwa FM Academia na Mashauzi Classic.
Bendi hizo
mbili – moja ya dansi na moja ya taarab – zikaumana vikali na kutoa burudani
iliyoacha gumzo kubwa.
FM Academia
ikiwa chini ya rais mpya Patcho Mwamba ikatandika sebene za nguvu huku Mashauzi
Classic iliyo chini ya malkia wa masauti Isha Mashauzi, ikitesa na ladha za
muziki wa pwani.

Hizi hapa ni
picha 15 za onyesho hilo la Mashauzi Classic na FM Academia lililohudhuriwa na
mashabiki wengi wa muziki.
 Waimbaji wa FM Academia jukwaani
 Isha Mashauzi jukwaani
Mashabi wakicheza wimbo “Nimpe Nani” kutoka kwa Isha Mashauzi
 Isha Mashauzi akitupia masauti yake matamu
 Kali Kitimoto wa Mashauzi akipapasa kinanda
 Kaposhoo akipiga tumba za FM
 Fred Manzaka kwenye kinanda cha FM
 Mpiga solo wa Mashauzi Classic Mkude Simba
 Waimbaji wa Mashauzi Classic Asia Mzinga (kushoto) na Rahma Aman
 Patcho Mwamba wa FM Academia na mmoja wa mashabiki wake
 Patcho Mwamba rais mpya wa FM Academia
 Rahma akiimba moja ya nyimbo za Mashauzi Classic
 Waimbaji wa FM Academia wakishambulia jukwaa
 Waimbaji wa FM Academia wakiendelea na makamuzi
 Hii ni sehemu ya mashabiki walioketi sehmu ya VIP ambayo kiingilio kilikuwa 15,000/=
 Sehemu ya eneo la viti vya kawaida ambayo kiingilio kilikuwa 10,000/=
 Muda wa kuua njaa …Kaposhoo akiachana na tumba zake na kwenda kucheza show
Kaposhoo akiendelea kusakata show

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *