PICHA 16 ZA SHEIKH ABUBAKARY KAULI ALIVYOZIKWA …Muft aongoza mazishi, wanasiasa washiriki


Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, jana aliongoza mazishi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Bakwata, Sheikh Abubakary Kauli aliyefariki usiku wa kuamkia Alhamisi.

Viongozi mbali mbali wa kisiasa, kidini, wafanyabiashara na wasanii mbali mbali, walishiriki mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu.

Vijana wa Kinondoni ambao walikuwa na huzuni kubwa ya kuondokewa na kipenzi chao, walikataa jeneza kubebwa na gari na badala yake walilibeba mabegani na kutembea nalo kwa mguu hadi makabauri ya Kisitu alikozikwa imamu huyo wa zamani wa msikiti wa Mtambani.

Katika hotuba iliyotolewa na Mufti nyumbani kwa marehemu Kinondoni mtaa wa Togo, kabla ya kuelekea makaburini, zikatajwa nyadhifa mbali mbali za Sheikh Abubakar Kauli, wasifu pamoja na historia iliyojaa vitu vingi vya kusisimua.
 Kisomo kikiendelea kabla ya kuelekea makaburini
 Mwanasiasa Idd Azan (kushoto) akiwa msibani na mfanyabiashara Eric Shigongo
Umati wa watu uliokuwepo mtaa wa Togo Kinondoni nyumbani kwa marehemu
 Mwili wa Sheikh Abubakary ukiwasili makaburi ya Kisutu
Kiongozi mkuu wa Jumuiya ya Bilal Muslim Sheikh Hemed Jalala na Muft wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeir wakiwasili makaburini
 Viongozi wa kiislam wakishiriki mazishi kwa huzuni kubwa
 Mazishi ya Sheikh Abubakary Kauli yakiendelea katika makaburi ya Kisutu
 Umati uliofika makaburini
 Taswira ya mazishi ya Sheikh Abubakary Kauli
 Hakika mazishi yalihudhuriwa na watu wengi sana
Hivi ndiyyo alivyozikwa Sheikh Abubakary Kauli
 Jopo la viongozi wa kiislam
 Muft wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry akitia mchanga kaburini
Sheikh Kundecha naye akishiriki kuzika
Mola amuweke mahala pema peponi Sheikh Ababubary Kauli


No comments