PICHA 25: CHARUKA KIPWANI ILVYOCHARUKA NDANI YA DAR LIVE J’MOSI USIKU …Jahazi, Zanzibar Stars, ‘sapraiz’ ya Five Stars wee wacha tu


Onyesho la Usiku wa Charuka Kipwani lililofanyika jana ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbalaga jijini Dar es Salaam, lilifana sana.

Burudani zilitandikwa kinoma noma huku kukiwa na mseto mtamu wa bendi za taarab na wasanii mbali mbali ingawa hakuna ubishi kuwa Jahazi Modern Taarab na Zanzibar Stars Modern Taarab ndizo zilizotawala zaidi onyesho hilo.

Bendi hizo mbili zilipanda jukwaani mara mara mbili kila moja huku upinzani wao wa kiaina uliojitokeza ukumbini kiasi cha baadhi ya wasanii kukunjana mashati, ukiongeza msisimko wa onyesho hilo.

Kulikuwa na ‘sapraiz’ ya iliyokuwa bendi ya Five Stars Modern Taarab, ambapo kibao “Riziki Mwanzo wa Chuki” kilichoimbwa na Chiriku Khadija Yussuf, kiliitikisa Dar Live.

Umati mkubwa uliofurika Dar Live pia ulipata uhondo kutoka kwa malkia wa mipasho Khadija Kopa ambaye kwa kawaida hafanyagi makosa kwenye maonyesho kama hayo.

Mkali wa miondoko ya kibao kata, Kivurande Junior naye aliupeleka puta ukumbi wa Dar Live, wakati Dullah Makabila alitesa kwenye miondoko ya Singeli.

Jike la Chui Hanifa Maulid naye alikuwa sehemu ya wasanii waliomimina uhondo adimu ndani ya Dar Live.


Pata picha kadhaa za onyesho hilo la Usiku wa Kucharuka Kipwani.
 Dullah Makabila (kushoto) akiwa na Kivurande Jr
 Dullah Makabila akifanya yake
 Fatma Kassim mmoja wa wasanii wa Jahazi waliofunika jana usiku
 Jumanne Ulaya "Vidole vya biashara" mpiga solo wa Jahazi
 Malkia Khadija Kopa akitesa na bendi yake ya Ogopa Kopa
 Chriku Khadija Yussuf akiimba mbele ya umati wa watu
 Khadija Yussuf jukwaani
 Khadija Yussuf akiimba "Rizki Mwanzo wa Chuki" aliotesa nao enzi za uhai wa Five Stars
 Kivurunde Jr mkali wa kibao kata
 Khadija Kopa jukwaani
 Khadija Kopa akiendeleza makamuzi
 Mohamed Mauji wa Yah TMK akilisabahi gitaa la solo la Jahazi kupitia wimbo "Tiba ya Mapenzi"
 Mauwa Teggo akiimba na Zanzibar Stars Modern Taarab
 Mkurugenzi wa Zanzibar Stars Juma Mbizo (kushoto) akiwa na viongozi wa Yah TMK  Muddy K (katikati) na Said Kessy Mnyama
Mishi Zele wa Jahazi
 Mishi Zele akitesa na wimbo wake "Nia Safi Hairogwi"
 Mosi Suleiman akiimba na Zanzibar Stars
 Mwasiti Kitoronto wa Jahazi akitesa na wimbo wake "Nataka Jibu"
 Umati uliofurika Dar Live
 Prince Amigo wa Jahazi akiliamsha dude
 Amigo akiimba "Tiba ya Mapenzi"
 Amigo na MC Dr Kumbuka wa Times FM
 Waimbaji wa Zanzibar Stars
 Captain Temba akimtunza Hanifa Maulid
 Jike la Chui Hanifa Maulid akiimba "Ishu Pambe"
 MC Muu (kushoto) akiwa na mwimbaji wa Zanzibar Stars Zena Mohamed
Zubeida Mlamali wa Jahazi akiimba na kundi la Zanzibar Stars

No comments