POLE SANA KING BLAISE KWA MSIBA WA MAMA YAKO MZAZI


Saluti5 inachukua fursa hii kutoa pole kwa mwimbaji nyota wa muziki wa dansi King Blaise kwa kufiwa na mama yake mzazi ambaye anatarajiwa kuzikwa huko kwao Congo Jumamosi hii.

King Blaise aliyetamba zaidi na bendi ya FM Academia, alifiwa na mama yake mzazi Jumanne iliyopita saa 9 mchana, Cape Town, Afrika Kusini alipokuwa akiishi na mwanae mkubwa.

Mungu ampe wepesi King Blaise katika msiba huu mkubwa pamoja na kumtakia ushiriki mwema wa mazishi ya mama yake kipenzi.

No comments