MWANAMITINDO na msanii wa Bongofleva, Siras Chassama "Q Boy Msafi" ambaye aliwahi kuwa msimamizi wa mwonekano wa staa wa muziki nchini Naseeb Abdul "Diamond Platnumz" amesema tayari amewahi kuwavisha mastaa wakubwa barani Afrika.

Q Boy ambaye hivi sasa anasimamia mwonekano wa msanii Young Dee, alisema kwa hapa nyumbani tayari amewahi kuwavisha wasanii kama Shetta, Harmonize, Rich Mavoko na wengine wengi.


“Mbali na Diamond, najivunia kufanya kazi na wasanii wakubwa Afrika, nimewahi kuwavisha P Square na Davido kipindi kile alipokuja Bongo, kwani ni hatua kubwa ambayo haiwezi kufutika kwenye historia yangu,” alisema Q Boy anayefanya vyema na wimbo wake, Karorero.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac