RAMADAN SOBHI ALAMBA MKATABA WA MIAKA MITANO STOKE CITY

WINGA wa Stoke City ambaye ni raia wa Misri, Ramadan Sobhi, ni kama ameula baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano ili kuitumikia klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 20, alijiunga na Stoke City majira ya joto yaliyopita akitokea katika timu ya Al Ahly, lakini akaweza kufanya makubwa katika michezo 19 aliyocheza wakati akiwa katika uangalizi.

“Hakuna shaka kuwa Ramadan ni kijana mwenye kipaji,” mkurugenzi mkuu mtendaji wa Stoke City, Tony Scholes, aliiambia tovuti ya klabu hiyo.

“Katika kipindi cha mwaka wake wa kwanza na akiwa katika Ligi mpya nikiwa mkweli naweza kusema ni kama umeingia kwenye utamaduni mpya na inakuwa ni changamoto kwa kila mchezaji,” aliongeza kigogo huyo.


Alisema kuwa haya hivyo Ramadan aliweza kuizoea Ligi hiyo na nchi kwa haraka na akawaonesha kuwa ni hazina muhimu.

No comments