RAMOS AFICHUA NAMNA NEYMAR ALIVYOMUAGA KUELEKEA PSG

STAA wa Real Madrid, Sergio Ramos ni kama amemkimbiza mwenzake wa Barcelona, Neymar baada ya kukiri akisema kuwa baada ya mechi yao ya mwishoni mwa wiki iliyopita ya Clasico alibadilishana naye jezi na kisha  akamweleza kuwa hataki kukutana naye tena akiwa kwenye uzi wa Barca.

Kwa sasa hatima ya Neymar kubaki Barca bado ni kitendawili, baada ya timu ya Paris Saint-Germains kuendelea kumfukuzia na huku ikimtangazia dau nono.

No comments