RASHFORD ASEMA MANCHESTER UNITED ILIPATA KINACHOSTAHILI


KWA kile ambacho unaweza kusema  ni kama ushindi umeanza kumpa kusema, straika Marcus Rashford amesisitiza kuwa Manchester United walipata kile walichostahili baada ya kufanya vyema majukumu yao na kushinda 2-0 dhidi ya Leicester City.

Mashetani Wekundu walilazimika kusubiri hadi dakika ya 70 kupata goli la kwanza katika uwanja wa Old Trafford baada ya kubanwa vizuri na Leicester.

Rashford ndiye mchezaji aliyekwamisha wavuni bao la kwanza baada ya Romelu Lukaku kukosa penalti, wakati Marouane Fellaini akiweka kimiani bao la pili.

Akizungumza na BT Sport baada ya mechi, Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekiri kuwa anafurahia kubeba uzito wa timu kwa kufunga goli muhimu kwa United.

"Tulitengeneza nafasi nyingi sana kipindi cha kwanza na ilionekana kama tungeshinda kama zile siku za nyuma," alisema. "Lakini timu iliendelea vema na jukumu na nashukuru tulipata goli. Ninapopata nafasi, najiamini nitafunga magoli."

United waliendelea kushinda bila kuruhusu goli katika mechi zao tatu za mwazo Ligi Kuu Uingereza kwa mara ya sita katika historia.

No comments