ROONEY MOTO CHINI AITUNGUA MANCHESTER CITY, STERLING ACHOMOA, MOURINHO ASHUHUDIA


Wayne Rooney amefunga bao lake la 200 la Premier League pale alipoifungia Everton katika mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya Manchester City kwenye dimba la Etihad.

Rooney alifunga bao hilo dakika ya 34 na kudumu hadi dakika ya 82 wakati Raheem Sterling alipoisawazishia Manchester City.

Timu zote zilimaliza zikiwa na wachezaji 10 baada ya Kyle Walker wa City kutolewa kwa kadi nyekundu (njano mbili) dakika ya 44 huku kiungo wa Everton Morgan Schneiderlin naye akilambwa kadi ya pili ya njano dakika ya 88.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho alikuwepo uwanjani kushuhudia mechi hiyo.

No comments