RUVU SHOOTING YAIVUTIA KASI SIMBA AGOSTI 26

TIMU ya Ruvu Shooting inatarajia kucheza mechi nne za kirafiki kabla haijakutana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Agosti 26, mwaka huu katika uwanja Uhuru, Dar es Salaam.

Jumamosi iliyopita walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi na kushinda bao 1-0 ikiwa ni mchezo wa pili baada ya ule wa Singida United Waliotoka sare yake ya 1-1.

Kocha wa timu hiyo, Abdulmutik Hadji alisema alivyokiangalia kikosi chakeka tika mechi hizo amebaini washambuliaji wake wana uchu wa mabao ila kuna sehemu anatakiwa kuwarekebisha wakae sawa.

Alisema kabla ya kuwavaa Simba atajitahidi kucheza mechi nne za kirafiki ili kushughulikia suala hilo pamoja na kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake kwa kuwajengea kujiamini na utulivu watakaposhuka dimbani siku hiyo.

“Beki yangu ya kati na straika ilikuwa haijatulia wanatupatupa mipira lakini nimeliona hilo nitalifanyia kazi ila katikamchezo wetu dhidi ya Yanga kila mchezaji ameonyesha silaha zake. Yanga wazuri na sisi tulikuwa vizuri pia,”alisema kocha huyo.


Alieleza kuwa kikosi chao ni kile kile cha msimu uliopita na wamefanya usajili wa mchezaji mmoja pekee Hamis Mcha kutoka Azam FC.

No comments