SAFARI YA KYLIAN MBAPPE KWENDA PSG IMEIVA


Inadaiwa kuwa Kylian Mbappe  amekamilisha vipimo vya afya tayari kwa usajili wake wa kujiunga na PSG akitokea Monaco.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18, amefanya vipimo vya afya huko Clairefontaine akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Usajili huo utahusisha mkopo wa msimu msimu kabla ya kuhamia jumla msimu ujao kwa dau linalokadiriwa kufikia pauni milioni 166.

No comments