SAIDA KAROLI APEWA SHAVU LA BONGOFLEVA

NYOTA mpya wa muziki wa kizazi kipya anayekuja kwa kasi kwenye miondoko hiyo, Mohammed Yahya ‘Peace Mapepe’ yuko mbioni kuachia kazi mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nakupenda’ ambayo amemshirikisha saida Karoli, imefahamika.

Hivi sasa mkali huyo anatamba vilivyo na ngoma zake mbili alizoziachia kati ya mwezi Machi na Mei, mwaka huu, ambazo ni ‘Macho Kodo’ na ‘Mdundiko’.

Akimnyetishia ripota wetu jijini Dar es Salaam jana, Peace amesema kuwa, pamoja na kwamba Saida amerudi kwenye ubora wake hivi sasa lakini pia amempa shavu kuzingatia ukaribu ulioko kati yao.


“Kabla ya kuachia kibao hicho, kwanza nitafyatua kitu cha ‘Namo’ ambacho nimewashirikisha Suma Mnazaleti na Pingu,” amesema Peace ambaye nje ya muziki ni mjasiriamali anayetengeneza na kuuza vipodozi vya asili kwa jumla na rejareja.

No comments