SANCHEZ AKUBALI KUMWAGA WINO ARSENAL NA KUVURUGA NDOTO ZA MAN CITY NA PSG KUMNASA

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger anakaribia kuzima ndoto za Manchester City na PSG kuinasa saini ya mshambuliaji wake, Alexis Sanchez baada ya kuwepo taarifa kuwa mchezaji huyo amekubali kusaini mkataba mpya wa dau la pauni 300,ooo kwa wiki.

Klabu hiyo zimekuwa katika mvutano mkali wa kutaka kuinasa saini ya mchezaji huyo ambaye amebakisha mkataba wake chini ya mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo.

Kwa muda mrefu, mchezaji huyo amekuwa akidengua kumwaga wino Arsenal ambayo ilianza kumpa pauni mil 225,000 lakini akizitolea nje vilevile.


Hata hivyo pamoja na Sanchez kukataa fedha hizo, aliwaweka wazi kuwa anataka pauni mil 300,000 na inaelezwa kuwa klabu hiyo imekubali yaishe.

No comments