SIMBA SC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini, Bidvest Wits katika mchezo uliofanyika uwanja wa Storrock Park, chuo kikuu cha Afrika Kusini katikati ya wiki.

Katika mchezo huo wa kujipima nguvu kujiandaa na msimu mpya, Simba SC walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni dakika ya 33, kabla ya mwenyeji kusawazisha.

Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kirafiki wa Simba katika kambi yake Afrika Kusini kujiandaa na msimu baada ya Jumamosi iliyopita kufungwa 1-0 na Orlando Pirates.


Baada ya mchezo huo, Simba SC inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kwa ajili ya mchezo mwingine wakujipima nguvu dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Agosti 8, mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac