SELEMAN KIBUTA AWEKA NADHIRI YA KUISAIDIA DODOMA FC KUPANDA DARAJA

STRAIKA mpya wa Dodoma FC, Seleman Kibuta, ameahidi atahakikisha anaisahidia timu hiyo kupanda daraja katika msimu wa 2018/19 Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania bara, Kibuta alikuwa kwenye kikosi cha majimaji na sasa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Dodoma FC inayojiandaa kushiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara (FDL) itakatoanza Septemba 16, mwaka huu.

Kibuta alisema kwamba atapambana kuhakikisha timu hiyo inacheza Ligi Kuu katika msimu huo.

“Nimekuja kwa kazi moja tu kuipandisha daraja timu hii kwani tuna kikosi kizuri mwalimu mzuri, Jamhuri Kiwelo, hivyo niwatoe hofu mashabiki kwa kuwaambia kwamba mambo mazuri yana kuja,” alisema Kibuta.

No comments