Habari

SELEMANI MATOLA ATHIBITISHA KUANZA MAZOEZI NA OMEGA, BUSUNGU KIKOSINI KWAKE

on

WACHEZAJI wa zamani wa Yanga, Omega Seme na mlinzi Busungu
wamejihakikishia maisha ndani ya kikosi cha Lipuli FC baada ya kusaini mkataba
wa miaka mmoja kwa kila mmoja.
Busungu aliyemaliza na Yanga msimu uliopita hakuweza kuongezewa
mkataba baada ya kushindwana na uongozi na hivyo kuwa mchezaji huru.
Kocha mkuu Lipuli FC, Seleman Matola alisema
tayari wachezaji wamesajiliwa na timu hiyo na kuungana na wenzao katika
kambi yao iliyopo Iringa.
“Tunashukuru mazungumzo yamekwenda vizuri, Busungu pamoja na
Omega ni wachezaji wetu halali na wameungana na wenzao Alhamisi kwenye mazoezi
ya kujiwinda na Ligi Kuu,” alisema Matola.
Aliongeza kikosi chake kitakua na wachezaji mchanganyiko
wakiwemo wakongwe ambao watasaidia kuimalisha timu hiyo ili iweze kukabiliana
na mikiki ya ushindani kwa timu kubwa.

Matola aliongeza baada ya wiki moja wanatarajia kuwa na mechi za
kirafiki dhidi ya Mbeya City, Njombe Mji pamoja na Singida United.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *