SERENA WILLIAMS ATABIRI KUJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

MCHEZA tenisI bora wa kike duniani, Serena Williams, ametabiri kuwa atajifungua mtoto wa kike hivi karibuni.

Serena aliandika maneno hayo mtandaoni, alipoweka picha ya kuonyesha mashabiki wake jinsi mimba yake ilivyokuwa, na kutabiri kuwa anahisi atajifungua mtoto mwenye jinsia ya kike.

"Nakumbuka wiki mbili baada ya kugundua kuwa nimepata ujauzito, nilicheza mechi ya Australian Open,” alisema Serena.


"Naamini ni mtoto wa kike kwa kuwa nakumbuka sikupata usumbufu wowote kwenye mchezo ule, nilitulia mno. Watoto wa kike huwa na tabia hiyo wanapokuwa tumboni,” alisema Serena huku akicheka.

No comments