SEYDON AENDELEA KUIPIGIA DEBE "SIO POA"

MKALI wa Bongofleva, Said Makamba ‘Seydon’ ameendelea kuwaangukia mashabiki wake kwa kuwaomba kuipakua kwa kasi kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Sio Poa’.

‘Sio Poa’ ambao kwa Seydon ni wimbo wake wa tatu aliouimba kwa kuwapa shavu Makomandoo, umebeba meseji kali juu ya wale wote wenye mienendo michafu kwa jamii akiwaambia ‘sio vizuri’.

“Ili nifike kule ninakokutaka lazima nipate sapoti kutoka kwa mashabiki, hivyo nichukue tu fursa hii kuwaomba wazidi kuupakua wimbo wangu huu kwa wingi zaidi,” amesema Seydon.


“Baada ya kazi hii ambayo nashukuru imekubalika mno, ninajipanga kuibuka na ujio mwingine mkali zaidi ambao nina hakika nao utakuwa funika mbaya,” ameongeza msanii huyo.

No comments