SHABIKI WA MUVI NIGERIA AOMBA KUFUNGA NDOA NA OMOTOLA JALADE

MITANDAO ya kijamii nchini Nigeria imekuwa sehemu muhimu kwa mashabiki wa fani ya uigizaji kuonyesha hisia zao za kimapenzi kwa mastaa wanaowakubali.

Hivi karibuni shabiki wa Omotola Jalade aliyejulikana kwa jina la Godwin Ahmed alituma ombi la kutaka kufunga ndoa na staa huyo pasipo kujali yupo kwenye uhusiano na rubani wa ndege Ekeinde.

Baada ya kuona ujumbe huo haujibiwi kwa muda mrefu akatuma ujumbe mwingine unaomchulia kifo staa huyo kutokana na kuchukizwa na maombi yake kutupwa kapuni.
Lakini hata hivyo Omotola ameendelea kuwa kimya na kupuuzia maoni ya shabiki wake.


Staa huyo anatajwa kuwa na mvuto wa kimapenzi kuliko waigizaji wengine wote wa Nollwood na ndoa yake imedumu kwa muda mrefu bila migongano.

No comments