SHAMSA FORD ATAKA WATOTO WANNE WA CHAPCHAP KWENYE NDOA YAKE

MKE wa mfanyabiashara wa nguo, Rashid Said “Chid Mapenzi”, Shamsa Ford  ameweka wazi kuwa baada ya kuishi katika ndoa kwa muda mrefu sasa anataka watoto wengine wanne.

Msanii huyo ambaye alifunga ndoa Septemba mwaka jana aliiambia Saluti5 kwamba ameshafanya mambo mbalimbali ya starehe na mume wake huyo na sasa umefika wakati wa kuongeza watoto wengine wanne ili idadi yao iwe watano.


“Kama kupendana tunapendana hivyo tunahitaji kupata watoto wanne zaidi katika ndoa yetu ili tuongeze furaha ya ndoa na watoto hao nitawazaa haraka ili niendelee na majukumu mengine ya kimaisha,” alisema Shamsa Ford.

No comments