SHOO KUBWA YA "USIKU WA SOTOJO" YAJA MAISHA BASEMET

JUMATANO ijayo inaweza kuwa ya kihistoria kwa mfalme wa Kibao Kata, Kivurande Junior pale atakapofanya mambo matatu makubwa ndani ya ukumbi wa Maisha Basemet, jijini Dar es Salaam.

“Siku hiyo kutakuwa na shoo kali niliyoipa jina la ‘Usiku wa Sotojo’ kwenye ukumbi huo sambamba na kusherehekea miaka mitano ya sanaa yangu ya muziki pamoja na Birthday Party yangu,” amesema Kivurande.

Kivurande amesema kuwa, kiingilio katika shoo hiyo ni sh. 10, 000 na 20, kwa viti maalum ambapo mashabiki 100 watakaowahi kuingia watazawadia CD mojamoja ya kibao ‘Moyo Kama Macho’ cha mkali huyo.


Amesema kuwa, wasanii kibao wa muziki Bongo wanatarajiwa kupamba shoo hiyo kubwa ya kwanza kwa mwaka huu ndani ya klabu hiyo, itakayoanza kuunguruma majira ya saa 3:00 usiku na kuendelea hadi asubuhi.

No comments