Habari

SHOW YA CHRISTIAN BELLA TABATA LEO USIKU NI ZAIDI YA TAMASHA …mastaa wa Bongo Movie, Bongo Fleva kupamba onyesho

on

Ni zaidi ya tamasha! Ndicho unachoweza kusema kuhusu onyesho la
Malaika Band chini ya Christian Bella litakalofanyika leo usiku ndani ya viwanja
vya BL Park Tabata Kinyerezi.
Mastaa kibao wa Bongo Movie na Bongo Fleva wamethibisha kushiriki
onyesho hilo ambalo ni maalum kwaajili ya utambulisho wa nyimbo tatu mpya za
Christian Bella.
Tayari jukwaa kubwa na la kisasa la onyesho hilo limeshakamilika
kufungwa tangu Alhamisi usiku, huku taa zenye nakshi nazo zikiwa zimekamilika
kufungwa Ijumaa usiku.
Vyoo vya kukodi (mobile toilets) tayari navyo vimeshafikishwa ukumbini
hapo ili kupanua wigo wa huduma hiyo muhimu kutokana na matarajio ya kufurika
kwa mashabiki wengi.
Mratibu wa onyesho hilo, Issa Mwendapole ameiambia Saluti5 kuwa hakuna
mshabiki atakayesimama kwa kukosa kiti. “Kutakuwa na viti na meza za kutosha,”
alisema Mwendapole.
Aidha, Mwendapole alisema eneo la VIP ambalo litalipiwa kiingilio cha
shilingi 20,000 litakuwa na meza kubwa na viti vya kisasa ambavyo vyote
vitanakshiwa na vitambaa vyeupe na visafi. Kiingilio kwa viti vya kawaida ni shilingi 10,000.
Meneja wa BL Park, Michael Masota naye amesema usalama utakuwa ni wa
hali ya juu kwa mashabiki na mali zao, huku vinywaji vya kila aina, nyama choma
na vyakula mbali mbali vikiwa ni sehemu ya huduma muhimu zitakazotolewa.
 Hivi ndivyo jukwaa la show ya Christian Bella lilivyokuwa linaonekana Ijumaa usiku baada ya kukamilika kufungwa
 Moja ya vyoo vya kukodi vikiwasili BL Park Ijumaa jioni
Hivi ndivyo kinavyoonekana choo cha kukodi kwa ndani

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *