SIKIA VITUKO VYA SERENA KWENYE UJAUZITO WAKE... eti ajitabiria kupata mtoto wa kike, kisa?

MCHEZA tenisi  Serena Williams, ametabiri kuwa atajifungua mtoto wa kike na ameeleza kinachomfanya kuamini hivyo.

Serena na mpenzi wake, Alexis Ohanian, wanaamini mtoto atakayezaliwa ni wa kike kwa kuwa mrembo huyo alishinda taji la Australian Open akiwa mjamzito.

Wawili hao hawataki kutumia teknolojia kujua jinsia ya mtoto wao, kwakuwa wanataka iwe "sapraiz".

“Bila shaka, alishinda Australian Open akiwa mjamzito. Hivyo, anaamini kuwa ‘dogo’ atakuwa msichana,” alisema Ohanian.

Kwa upande mwingine, Serena ameonyesha kuwa ni mwanamke wa shoka, kwani licha ya kitumbo chake, ametupia picha kwenye mitandao ya kijamii inayomwonyesha akifanya mazoezi.


Mrembo huyo anatarajiwa kujifungua mwishoni mwa mwezi huu, lakini ameendelea na mazoezi yake ya ‘gym’ kama kawaida.

No comments