SIKILIZA RHUMBA BAB KUBWA LA BIMA TAARAB KATIKA KITU "I LOVE YOU" CHA MARIAM NAYLON


MNAMO mwaka 1988 kwenda 89, bendi ya mipasho ya Bima Modern Taarab iliachia albamu yao inayokwenda kwa jina la “Kijiba cha Moyo” na ndani yake kukawa na vibao takriban sita, kimojawapo kikiwa ni “I Love You”.

“Bosanova” ndio miondoko  iliotumika katika wimbo huu ambao umetungwa na Ally Tajiruna na mwimbaji akiwa ni Mariam Naylon ambao wote ni marehemu kwa sasa.

Baadhi ya walioshiriki kuirekodi kazi hii ya takriban dakika 7.31 ni Msuya Mselem amesimama kwenye gitaa la solo na Hamis Shaaban Mandevu (bass), huku kinanda kikiwa kimepapaswa na mkali Ally Hemed “Star”.


Mpangilio safi wa mashairi, ala na sauti ya kutetemeka ya bibie Mariam ni kati ya vivutio vikubwa ndani ya wimbo huu ulioimbwa kwa mchanganyiko wa lugha mbili za Kiswahili na Kiingereza ili kusisitiza “mahaba mubashara” kwa anayelengwa.

No comments