Safari ya ZLATAN IBRAHIMOVIC kurejea Manchester United ipo karibu mno ambapo wadhamini wa jezi zao -Adidas - tayari wamevujisha jezi yenye jina lake.
Mshambuliaji huyo anayepona kwa kasi maumivu yake ya goti, yuko mazungumzoni na  Manchester United katika dili la mkataba wa msimu mzima. 
Jezi iliyovujishwa inaonyesha Ibrahimovic atavaa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Wayne Rooney.
Hapo kabla katika msimu uliopita, Ibrahimovic alikuwa akivaa jezi namba 9 ambayo imechukuliwa na Romelu Lukaku.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac