SNOOP DOGG ACHUKIA MWONEKANO WAKE WA KIHUNI

Rapa mkorofi Snoop Dogg amesema kuwa moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakimtatiza ni kutazama kazi zake ambazo amewahi kuzirekodi kipindi cha nyuma.

Rapa huyo ambaye amekuwa akishtumiwa kwa kutumia bangi kwa kiwango kikubwa amesema kuwa video nyingi alizocheza miaka ya nyuma alikuwa na mwonekano wa kihuni mbele ya jamii.

“Nadhani kila mmoja anaona namna ambavyo nimebadili mfumo wa maisha yangu lakini nimekuwa nikihukumiwa na matukio ya nyuma,” alisema rapa huyo.


“Huwa inanipa shida kidogoo kutazama video zangu za miaka ya nyuma kwa sababu najua jamii inanichukulia vilevile,” aliongeza.

No comments