“SOGEA UYAJUE” GUMZO AFRICA SWAHILI TV

KIPINDI cha ‘Sogea Uyajue’ kinachorushwa katika runinga ya Africa Swahili Tv kila Jumanne saa 7:10 mchana na kurudiwa Alhamisi muda kama huo, kimeonekana kuzidi kukubalika.

Baadhi ya watazamaji waliopiga stori na ripota wetu wamesema kuwa, wanafurahishwa zaidi na waendeshaji wa kipindi hicho ambao ni wanadada wawili wanaojulikana kama Super Modo na Dodo wanaoonekana kunogesha vilivyo.

“Kiukweli ‘Sogea Uyajue’ ni kipindi ambacho binafsi nakikubali sana kwasababu licha ya kutoa burudani lakini pia kinaelimisha jamii, hususan kuhusiana na mazingira yanayotuzunguuka,” amesema mmoja wa watazamaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Ally Jangalu.

Jangalu ameongeza kusema kuwa anawaomba waandaaji wa kipindi hicho kuzidisha vinogesho ili kukifanya kipindi hicho kuwa habari ya mjini zaidi na kuvuta watazamaji wengi kupita ilivyo sasa.

No comments