TAMBWE AWAAMBIA WANA YANGA "TULIENI MUONE, TAMBO ZA SIMBA MWISHO AGOSTI 23"

MSHAMBULIAJI mkongwe wa Yanga, Amissi Tambwe amewashusha presha mashabiki wao akisema wasiwe na wasiwasi na Simba aliyoiona na kwamba watulie waone mambo makubwa Agosti 23 watakapowanyamazisha.

Tambwe alisema wameiona Simba lakini haijawashtua hata kidogo na kwamba wanaingia kambini Zanzibar kisha wakirudi wanakuja kuharibu hali ya hewa katika kambi ya watani wao hao.

Tambwe amesema anafurahi kuona mashabiki wa Simba wamekuwa na uhakika mkubwa kwamba watawafunga na kwamba hilo litawajaza matumani watani wao hao na kuingia katika mchezo huo kwa uhakika, hatua ambayo itawapa wakati mgumu.

Alisema, hana wasiwasi na kikosi chao na kwamba uongozi wa benchi la ufundi umesajili kisayansi ambapo hadi sasa kocha wao bado alikuwa akiwasoma wachezaji wote na sasa anaamini anakwenda kumaliza kazi katika kambi yao ya Zanzibar.

“Mimi sioni sababu ya kuihofia Simba, hata mimi nimeiona wala haijanishtua. Unajua wachezaji tunajua wachezaji viwango vyetu havija tofautiana sana,” alisema Tambwe.


“Unajua hata mimi jana (Jumamosio) sikucheza, kocha aliniambia kabisa kwamba hatanichezesha, kuna kitu anataka kukiangalia na Simba nikiiangalia wala hainipi wasiwasi tutawala mapema kabisa watu hawataamini, wamejiamini sana na hilo ndiyo zuri kwetu."

No comments