TAMBWE AWAITA MASHABIKI KUSHUHUDIA MNYAMA ANAVYOCHINJWA TAIFA KESHO

MSHAMBULIAJI wa Yanga Amissi Tambwe ameombwa aanzie benchi ili akiingia awamalize Simba lakini akawaambia mashabiki wa Yanga wala wasiingie baridi waje kwa wingi na kwamba Simba hawatoki  kwa vyovyote.

Akizungumza na Saluti5, Tambwe amesema kwa sasa ameridhika na kikosi chao na kipo tayari kutoa dozi yoyote na kwa kuanzia Simba watakuwa na kazi kuwazuia katika mchezo wa kesho baina ya timu hizo.

Tambwe ambaye hakauki kuifunga Simba, amesema ameridhika na mbimu za kocha Geogre Lwandamina na kwamba anavyowajua Simba watapata taabu na akili hizo za Mzambia huyo.

Alisema kwa sasa kikosi chao kina jeuri kubwa kutokana na kila mchezaji kuwa katika kiwango bora, jeuri ambayo imekuwa ikiwawezesha kuifunga timu yoyote na kuwataka mashabiki wa Yanga kuja kwa wingi kuwapa nguvu.

“Sioni sababu ya mashabiki wa Yanga kuwaogopa Simba sasa, naamini tupo tayari niwaambie tu waje kwa wingi kama kawaida Simba hawatatoka salama kwetu, hatutaki kuongea sana,” alisema Tambwe.


“Tumefanya maandalizi ya kutosha na kwa sasa kila mchezaji ana hamu na hiyo mechi, ninavyoijua Simba watapata tabu sana kutuzuia tutawafunga tu hawataamini na majina yao."

No comments