TANZANIA PRISONS YAJIFICHA KISIWANI ZANZIBAR MAANDALIZI YA LIGI KUU

KUELEKEA msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara, maafande wa Tanzania Prison wamekwenda kuweka kambi Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Akizungumza jana beki wa kulia wa klabu hiyo, Salum kimenya, amesema maandalizi yanakwenda vizuri na hadi sasa wanaendelea na program ya mazoezi chini ya kocha Mohamed Bares.

“Ni kambi nzuri sana, unajua unapobadili mazingira unajifunza mengi, naamini tutakuwa bora zaidi msimu mpya utakapoanza kwani mazoezi tuliyofanya ni ya hali ya juu,” alisema.

Alisema kuwa aina ya wachezaji wapya walioongezwa itaongeza chachu katika kikosi chao hicho ambacho msimu uliopita hakikuwa katika hali nzuri kutokana na kupata matokeo yasiyoridhisha.


Wajelajela hao watafungua pazia la Ligi kuu wakiwa ugenini Njombe kukipiga na timu iliyopanda daraja ya Njombe Mji, ambayo imekuwa tishio katika siku za karibuni katika michezo ya maandalizi.

No comments