Habari

THIERRY HENRY ASEMA ARSENAL HAITAZAMIKI NA HAISTAHILI KUTAZAMWA

on

NYOTA wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry, ameonekana
kukerwa na kiwango kilichooneshwa na Gunners katika mchezo wao wa juzi ambao
waliambulia kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Liverpool na ameamua kuipa jina kama
timu ambayo haifai kuangaliwa mechi zake.
 Katika mchezo huo wa juzi kikosi hicho cha Arsene Wenger
kilionekana kufa kabisa kwenye safu ya kiungo wa kati hali ambayo iliwapa
nafasi  Liverpool kutakata kwa kutumia mashambulizi ya
kushtukiza  yaliyowafanya waondoke kifua mbele kwenye dimba lao
la Anfield.
Walikuwa ni
wachezaji, Roberto Firmino  na  Daniel Sturridge, waliokuwa
wakitamba katika eneo la hatari na huku  Sadio
Mane  na  Mohamed Salah nao wakionekana kutamba kwa
kukimbia na mpira kutoka upande mmoja hadi mwingine kutokana na kukosekana mtu
wakuwadhibiti.
Kutokana na hali hiyo, Henry alisema juzi kwamba hawezi
kuendelea kuzitazama mechi za timu yake hiyo ya zamani baada ya kushuhudia
jinsi ilivyopasuliwa na vijana hao wa Jurgen Klopp.
“Hii ni timu ambayo haistahili kuangaliwa. Ilifika wakati
fulani nilitaka kuondoka uwanjani. Ni vigumu kuvumilia,”
alisema  Henry katika mahojiano na Sky Sports.

“Sijafurahishwa
na timu na sidhani kama mashabiki wote hawapo hivyo. Hili ni tatizo. Arsenal
kulikuwapo na utulivu na hii si presha ambayo mtu unatakiwa kuwa nayo kwenye
klabu kubwa kama hii,” aliongeza Mfaransa huyo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *