THOMAS LEMAR ASEMA BORA KUSAJILIWA MAN UNITED KULIKO ARSENAL


MANCHESTER UNITED imepewa 'shavu' la kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar anayewaniwa kwa udi na uvumba na Arsenal.
Mwandishi anayeaminika Duncan Castles ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 angependelea kujiunga na Manchester United kuliko Arsenal.
Arsene Wenger amekuwa akimsaka Lemar kwa dirisha lote la kiangazi lakini sasa kocha huyo wa Arsenal amekiri kukata tamaa.
Wenger anasema: "Mpango huo umekufa kwasababu Monaco hawataki kumuuza.
“Kylian Mbappe, Fabinho wako mbioni kuondoka. Wamewapoteza Benjamin Mendy, Bernardo Silva, Tiemoue Bakayoko. Naamini Monaco wako kwenye hatua ambayo haiwaruhusu kuuza mchezaji mwingine."

No comments