THOMAS MULLER ASEMA RODRIGUEZ SIO MSHINDANI WAKE

STRAIKA Thomas Muller amesititiza kuwa haoni kama mchezaji mpya wa Bayern Munich, James Rodriguez atakuwa mshindani wake katika kupigania namba kwenye kikosi cha kwanza na badala yake akasema kuwa atahakikisha uchekaji wake  na nyavu unaendelea kuwa palepale.

Straika huyo anasema pia amefurahishiwa na ujio huo wa James ambaye amewahi kucheza naye kwa muda wa miaka wakatiu akikipiga kwa mkopo akitokea Real Madrid.

Msimu uliopita Muller aliweza kufunga mabaoa matano katika harakati zake za kutafuta mfungaji bora kwa mara ya sita  katika michuano  ya Bundesliga,lakini amekuwa akicheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.

Hata hivyo anasema kuwa haoni kama kuna tishio kutoka kwa James  na mwenzake Corentin Tolisso, ambaye amesajiliwa akitokea Lyon kwa mkataba ambao gharama yake inaweza kufikia Euro milioni 47.5.

Pia kocha wao, Carlo Ancelotti tayari ameshakanusha uvumi unaodaia kuwa ujio wa  James unaweza kumfanya  Muller akapoteza namba.


Akizungumza juzi, Mjerumani huyo alisema kuwa ana uhakika wanaweza kucheza kwa pamoja  na huku akisema kuwa kwa mtazamo wake  James  na Tolisso wanaweza kuwa washirika wako na si washindani  na ataweza kutekeleza majukumu yake kadri kocha wake atakavyohitaji.

No comments