TIFFANY AFANYA UPASUAJI MARA KUMI NA TATU KUTAFUTA MUONEKANO WA IVANKA TRUMP

MREMBO wa Marekani, Tiffany ameripotiwa kufanya upasuaji wa mwili wake mara kumi na tatu ili aweze kufanana na Ivanka Trump ambaye ni mtoto wa rais wa taifa hilo.

Upasuaji huo mara 13 wote umefanyika ndani ya mwaka mmoja ikiwa kama sehemu za jitihada zake ili aweze kuwa na mwonekano kama wa Ivanka.

Kabla ya kufanyiwa upasuaji huo, Tiffany alikuwa akiamini kuwa hakuna mrembo mwenye mvuto kumzidi mtoto wa Trump Duniani.

“Navutiwa na Ivanka, yeye ni mwanamke wa mfano kwangu, najaribu kufanya kile anachofanya,” alisema Tiffaany.

No comments