TIMBULO AFUNGUKA JUU YA UKIMYA WAKE

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Ally Timbulo  amesema ukimya wake wa muda mrefu ulilenga kujifunza na kuangalia kazi za wasanii wengine.

Timbulo alisema hivi sasa amejipanga kuendelea kuachia kazi mpya ili kuziba mapengo ya nyuma.

Alisema ukimya wake umeweza kumsaidia kulisoma soko la muziki wa Tanzania hivyo amepata urahisi wa kundaa kazi zake na kupanga muda sahihi wa kuziachia.

“Kuna kipindi nilikuwa kimya sana, watu walifikiri nimeacha muziki na kugeukia shughuli nyingine lakini hawakujua kuwa niliamua kufanya vile kwa makusudi,” alisema Timbulo.


Msanii huyo alieleza kuwa mipango yake ni kuwa miongoni mwa wasanii watakaofanya kazi bora zaidi mwaka huu na miaka ijayo.

No comments