TSHISHIMBI KUMLETA BEKI KIBOKO YA WASHAMBULIAJI WA SIMBA

YANGA imeambiwa itulie na kwamba kiungo wao mpya Kabamba Tshishimbi amewaambia usajili wa mwezi Desemba atamvuta beki wa maana atakaekuja kuzima kelele za washambuliaji wa Simba.

Taarifa kutoka ndani Yanga ni kwamba mabosi wa timu hiyo walimuelezea kiungo huyo juu ya kuhitaji beki wa maana mwenye uwezo wa kukaba mpaka vivuli na kutakiwa kutulia waletewe mtu wa maana.

Mmoja wa mabosi wa klabu hiyo alisema Tshishimbi amwaaambia kuanzia sasa ameshaanza kumpanga beki huyo rafiki yake ili aje kuungana nae katika kikosi hicho ambaye ana uwezo mkubwa wa kuwakomesha washambuliaji wabishi.

Bosi huyo alisema Tshishimbi amewaambia amewaona washambuliaji wa Simba katika michezo ya kirafiki na kwamba hana wasiwasi kwamba akitua tu baada ya kumalizana na viongozi wa Yanga washambuliaji wa Simba watakimbia mziki wake.

“Tulimwaambia tulikuwa tunatafakari kwamba tulikuwa tunatafuta beki wa maana akasikitika sana akatuambia tutulie angejua mapema angeshatuletea hata kabla ya yeye kufika hapa Yanga,” alisema bosi huyo.


“Ametuambia kwamba ameanza tayari kazi ya kumpanga huyo beki ili aje hapa na amewaona washambuliaji wa Simba akatuambia hawana jipya endapo beki huyo atafika.

No comments