MATAJIRI Yanga hawataki utani na katika kuhakikisha kiungo wao Papy Kabamba Tshishimbi hapati shida wamejitolea kumpa nyumba ya maana.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kwamba Tshishimbi amepewa nyumba ya maana na ya kisasa maeneo ya Masaki ikiwa na ulinzi mkali.

Bosi mmoja wa Yanga amesema nyumba hiyo ya Tshishimbi amekabidhiwa na tajiri mmoja wa Yanga ambaye ametaka kuona kiungo huyo anafanya kazi yake kwa utulivu.

Nyumba hiyo yenye kila kitu ndani uchunguzi umeonyesha imezifunika zile walizokabidhiwa mastaa wakubwa wa Simba kama Emmamuel Okwi na Haruna Niyonzima ambaye bado inadaiwa kutumia nyumba iliyokuwa akilipiwa na Yanga maeneo ya Kijitonyama.

Mbali na nyumba hiyo, Tshishimbi pia anatumia gari la maana aina ya Ford Ranger yenye thamani ya sh mil 90.

“Tumeona tumfanyie makubwa kiungo wetu na hawa wanaofanya hivi ni matajiri wetu ambao wameamua kukaa nao kuona huyu mtu hapati tatizo ili afanye kazi yake kwa utulivu,” alisema bosi huyo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac