TWANGA PEPETA YAACHANA NA SHOW ZA CLUB MASAI KILA JUMATANO


Bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta” imeagana rasmi na ukumbi wa Meriadian Hotel (Club Masai) ambapo ilikuwa ikipatikana kila Jumatano.

Akiongea na Saluti5, mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka akasema kuanzia Jumatano ya wiki hii hawatakuwepo Club Masai Kinondoni na badala yake watatafuta kiwanja kingine.

Asha Baraka amesema hatua hiyo imefuatia lengo lao la kupunguza maonyesho yanayokaribiana ambapo mbali na kupiga Club Masai pia walikuwa wanapatikana Mango Garden kila Jumamosi. Kumbi hizo mbili ziko pua na mdomo.

“Tumeyafanyia kazi maoni ya mashabiki wetu na sasa tumeamua tuwe na onyesho moja tu kwa wiki ndani ya Kinondoni,” alisema Asha Baraka.

No comments