USAIN BOLT ASEMA NUSURA AMWAGE CHOZI AKIHITIMISHA NGWE YAKE

MKIMBIZA upepo mahiri, Usain Bolt, amesema ilibaki kidogo amwage chozi wakati akihitimisha ngwe yake majuzi katika kibarua hicho kutokana na kwamba ilikuwa ni kama anasema kwa heri kwa kila kitu.

Staa huyo alihitimisha kibarua hicho katika mashindano ya kuwania ubingwa wa dunia jijini London ikiwa ni baada ya kuwa mshindi wa dhahabu mara nane katika michuano ya Olimpiki na huku akiwa amekizolea sifa nyingi katika mchezo huo.

“Inasikitisha kwamba inanilazimu kuondoka sasa,” alisema raia huyo wa Jamaica, ambaye alikiambia kuzungumza uwanja kuwaaga wachezaj waliokuwapo uwanjani jijini London Jumapili usiku wa kufungwa kwa mashindano hayo.

“Nilikuwa nasema kwaheri kwa mashabiki kwa mashindano niliyokuwa nashiriki pia,” aliongeza.

Alipoulizwa iwapo atarejea kushindana tena alijibu : “Nimewaona watu wengi sana wakistaafu na kurudi tena halafu hali yao inakuwa mbaya zaidi au wanajiaibisha sitakuwa mmoja wa watu hao.”


Bolt alishinda shaba mbio zake za mwisho za mita 100, kasha akumia na kushindwa kumaliza mbio za kupokezana vijiti za 4x100 jumamosi usiku.

No comments