USAIN BOLT AWAUMBUA WANAODAI AMEJIFANYISHA KUUMIA KWENYE MBIO ZA LONDON MARATHON

USAIN Bolt ameibuka na kuwachana wale waliokuwa wakimbeza kuwa alijifanyisha kuumia ili kukwepa aibu ya kupoteza mbio zake za mwisho, kwenye London Marathon.

Mjamaica huyo mwenye rekodi lukuki kwenye riadha, alilazimika kuweka picha ya jeraha lake la msuli kwenye mtandao wa Twitter ili kuthibitisha kuwa ni kweli aliumia.

"Nimesikitika mno na taarifa hizo. Miezi mitatu iliyopita nilifanyiwa vipimo na kubaini tatizo langu, lakini sikubadili mawazo yangu ya kushiriki mbio za London,” alisema Bolt.


"Mimi si mtu wa kuweka hadharani mambo yangu, lakini nimelazimika baada ya kuona watu wakihoji kama ni kweli niliumia au la. Nawaheshimu sana mashabiki zangu, siwezi kuwadanganya.”

No comments