USHINDI DHIDI YA DORTMUND WAMPA KIDOMODOMO ANCELOTTI

KOCHA Carlo Ancelotti amesema kwamba ana uhakika kikosi chake cha Bayern Munich  kitafanya vizuri katika michuano ya Bundesliga, baada ya kuwachapa mahasimu wao  Borussia Dortmund  katika mchezo kufungua msimu wa Kombe la DFL-Supercup.

Bayern walitinga katika michezo huo uliopigwa katika Uwanja wa  Signal Iduna Park  wakiwa na kumbukumbu ya kupokea vipigo vinne katika michezo ya kirafiki vikiwamo vikubwa viwili ilivyovipata kutoka kwa  timu za AC Milan na Liverpool.

Hata hivyo vinara hao walijikuta wakilazimika kuwa nyuma mara mbili katika mchezo huo wa  Klassiker, lakini Robert Lewandowski  akaweza kusawazisha la kwanza walililodungwa na Christian Pulisic na kisha  Roman Burki' akajifungwa kwa bahati mbaya zikiwa ni dakika  na huvyo kumfanya Pierre-Emerick Aubameyang kuondoka akiitwa staa wa mechi.]

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Ancelotti aliwaambia waandishi wa habari kwamba anatarajia Bayern watazinduka na kufanya vizuri kuanzia mchezo wao wa kwanza  wa Ligi ya  Bundesliga  dhudi ya  Bayer Leverkusen.


"Ni sawa ubingwa ndio kitu cha muhimu," alisema kocha huyo. "Nimelizika tumecheza kwa utulivu wa hali yajuu. Manadalizi yetu ya msimu ujao  hayakuwa mazuri, lakini hatuhitaji kuwa na hofu na msimu utakapoanza tutakuwa tayari kwa hilo,”aliongeza Ancelotti.

No comments