VIPIGO VIWILI VYA REAL MADRID VYAMNYONG'ONYESHA GERARD PIQUE

BEKI wa Barcelona, Gerard Pique amesema kwamba amejisikia amenyong’onyea kutokana na vipigo viwili walivyovipata kutoka kwa Real Madrid kwa mara ya kwanza katika michuano ya Kombe la Spanish Super Cup.

Kauli ya staa huyo imekuja baada ya mabingwa hao wa LaLiga na Ulaya usiku wa Jumatano kuondoka na ushindi wa mabao 2-0 na hivyo kuhitimisha ushindi wa jumla ya mabao 5-1.

Kutokana na vipigo hivyo, Pique mwenye umri wa miaka 30 ambaye ameitumikia Barca kwa muda wa miaka tisa alisema mara baada ya mchezo huo kwa sasa wapo katika kipindi kigumu kama timu na klabu.

“Tupo katika kipindi kigumu kama timu na klabu. Huu ni mchakato mrefu na tuna nafasi ya kujiimarisha, ni lazima tuwe watulivu na kuangali ya mbeleni,” alisema staa huyo.


Katika mchezo huo Real Madrid haikuwa na nyota wake, cristiano Ronaldo ambaye amefungiwa kucheza mechi tano, baada ya kupewa kadi nyukendu katika mchezo wa kwanza na iliwaweka benchi mastaa wengine Gareth Bale na Isco.

No comments