WENGER AMCHEKA ANTONIO CONTE ANAYELIALIA NA "UDOGO" WA KIKOSI CHAKE

ARSENE Wenger amemwambia kocha wa Chelsea, Antonio Conte kuacha kulialia kwamba ana kikosi kidogo.

Kocha huyo wa Arsenal, Wenger alisema Conte na mabosi wake wa Chelsea wanapaswa kujilaumu wenyewe kutokana na kuwatoa kwa mkopo wachezaji wao wengi.

Conte amekuwa akilalamika kushindwa kufanya usajili kukiboresha kikosi chake ndicho chanzo cha mipigo cha mikwaju ya penalti kutoka kwa Arsenal katika mchezo wa ngao ya jamii.

Hata hivyo Wenger ambaye kikosi chake kilianza msimu mpya wa Ligi Kuu England usiku wa juzi Ijumaa kwa kumenyana Leicester City huko Emirates, alisema: 

“Niwaonee huruma Chelsea kwa sababu eti hawana wachezaji wengi? Hilo halipo. Ukitazama idadi ya wachezaji wao waliowatoa kwa mkopo, wanaweza kuwarudisha baadhi yao kikosini.”

Kocha Wenger alisema bado anawatazama wachezaji wapya wa kuwasajili katika kikosi chake katika dirisha hili.

“Bado tunasajili, hata hivyo ni wazi kwa kipindi hiki nina wachezaji 33 hivyo inakuwa kazi ngumu kuwaongoza wachezaji wengi katika shughuli za kila siku,” alisema Wenger.


Wakati huohuo, Wenger amekana kuwa kikosi chake kilikaribia kabisa kumnasa staa wa Leicester City, Riyad Mahrez anayetajwa kuwa na thamani ya pauni mil 40.

No comments