WENGER ASEMA ARSENAL YA MSIMU HUU MWENDO MDUNDO

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amejinasibu kuwa kikosi chake cha msimu huu kitafanya maajabu katika Premier League.
Wenger amesema licha ya kufanya usajili mdogo, lakini anaamini mshikamano uliopo kati ya wachezaji wake, utachangia timu kufanya vizuri.
Kocha huyo anasema ushindi wa Ngao ya Hisani dhidi ya Chelsea, nao umeongeza ari ndani ya timu.
Arsenal inategemewa kuanza kampeni za kusaka taji la Premier League wikiendi hii dhidi ya mabingwa wa mwaka juzi, Leicester City.

No comments