WENGER AWATOA HOFU MASHABIKI WA ARSENAL KUHUSU TAARIFA ZA KUUMIA KWA LACAZETTE

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amewatoa wasiwasi mashabiki kuhusu taarifa zinazodai kuwa nyota wao, Alexandre Lacazette aliumia juzi katika mchezo wao wa Kombe la  Emirates ambao walifungwa na  Sevilla.

Staa huyo aliyasajiliwa bei mbaya na Arsenal juzi alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza akiwa kwenye uwanja huo wa  Emirates, baada ya kuunganisha krosi  kutoka kwa Alex Oxlade-Chamberlain likiwa ni la kufuta  la kwanza lililofingwa na Joaquin Correa, lakini Steven N'Zonzi akaongeza la pili lililoifanya  Sevilla  kuondoka na ushindi  wa mabao  2-1.

Baada ya kufunga bao hilo straika huyo  alipumzishwa zikiwa zimebaki dakika 12 kabla ya mpira kumalizika na nafasi yake ikachukuliwa na Alex Iwobi  huku  wakati akiondoka uwanjani alionekana akichechemea.

Hata hivyo  pamoja na hali hiyo, Wenger alikanusha kuhusu staa huyo wa timu ya Taifa ya Ufaransa kuwa aliumia na huku akisisitiza kuwa yupo fiti.

"Lacazette yupo fiti," Wenger aliwaambia waandishi wa habari. "Nilimpumzisha lakini sio kwa sababu alipata majeraha ni mmoja kati ya wachezaji ambao  kwa leo (juzi) mpira uliwakataa,”aliongeza Mfaransa huyo.

"Nimevutiwa na kiwango kilichooneshwa na  Lacazette. Alikabiliwa na ugumu wakati tulipokuwa tumebanwa.Lakini unapoweza kufunga bao lako la kwanza ukiwa  Emirates hali huwa inakuwa tofauti kwako,”Wenger aliongeza zaidi.

No comments