WIZKID AACHIA NGOMA YAKE ALIYOMSHIRIKISHA 2FACE

MSANII Wizkid ametimiza ahadi yake juzi Jumatatu, ya kuachia ngoma yake mpya aliyofanya na mkongwe wa muziki nchini Nigeria, 2 Face.

Wiz alitoa taarifa za kuachia wimbo huo uitwao “Medicene” kuanzia Jumapili hii kupitia mtandao wa Twitter. 

Mkali huyo wa “Come Closer” yupo mbioni kuachia ngoma yake nyingine aliyofanya na mwanadada Tiwa Savage.

Wakati huo huo muimbaji huyo ametajwa kutumia masaa 48 ambayo ni sawa na siku mbili kuandaa albamu yake mpya anayotarajiwa kutoka siku yoyote kuanzia sasa.   

No comments