YAH TMK WAJA NA USIKU WA MAMBO YA PWANI DAR LIVE KILA JUMATANO


Kuanzia Jumatano hii na kila Jumatano, kundi la Yah TMK Modern Taarab litakuwa likitupia burudani zake ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Meneja wa kundi hilo, Muddy K Usher, ameiambia Saluti5 kuwa kuanzia Jumatano hii watakuwa wakipatikana Dar Live katika show itakayojulikana kama “Usiku wa Mambo ya Pwani”.

Muddy K amesema watakuwa wakisindikizwa na kundi la bongo fleva la Madada Sita huku kiingilio kwa wanawake kikiwa ni bure (Ladies Free).

No comments